Tulipata kuandika kuhusu “Bismillah” katika kitabu
chetu cha MAMBO YA MSINGI YA UISLAM katika
uchambuzi wa suratul Fatiha; vile vile ndani ya
makala yenye kichwa “RAHMAN - RAHIM”.
Hapa
tutaangalia upande wake mwingine...
Inafahamika kwamba katika swala za jamaa pamoja na
ukweli wa kwamba bismillah ndiyo aya ya mwanzo ya
suratul Fatiha, huwa haisomwi kwa sauti na imam!
Imam huwa anaanza kusoma kwa sauti moja kwa
moja kuanzia na “alhamdulillahirabbil’alamiyn”
Je ni kwa nini Imamu huwa hasomi bismillah kwa
sauti pamoja na kuwa ndiyo aya ya kwanza ya
suratul fatiha na kusoma kwa sauti kuanzia aya ya
pili? Na hapo maamuma wanaisoma kimoyomoyo(!) eti
kukamilisha mapungufu yake(!)
Kwanza ngoja
tugusie kwa kifupi jambo ambalo lilijadiliwa
zamani.
Wapo waliosema kwamba suratul
fatiha ina aya 7; na wapo waliosema kwamba aya ya
kwanza ya suratul fatiha
“alhamdulillahirabbil’alamiyn” na kwamba bismillah
ya mwanzo imewekwa kama kianzilishi tuu.
Wale waliozama katika jambo hili kwa undani
wamefikia maoni ya kwamba bismillah ndiyo aya ya
kwanza ya suratul fatiha.
Na wengi wetuı
hii leo tunamaoni kama hayo.
Hali ikiwa ni
hiyo jambo linalotuvutia kwanza ni hili
lifuatalo...
Kwa nini baada ya kusema
“Rahmanirrahim” pamoja na Bismillah, ikarudiwa
tena baada ya “alhamdulillahirabbil’alamiyn”?
Hatutoingia katika mjadala huu hapa. Lakini
kutokana na umihimu wa jambo hili tunataka kugusia
kwa mara nyingine hizi aya mbili kama ifuatavyo:
1. “Bismillahir Rahmanirrahim” 2.
alhamdulillahirabbil’alamiyner Rahmanirrahim
Siri iliyopo hapa tumejaribu kuieleza katika
makala yetu ya “RAHMAN - RAHIM” kwa kadiri maneno
yalivyo ruhusu.
Kwa mujibu wa ukweli huo,
tunalotakiwa tulifahamu ni:
Ili swala
igeuke kuwa Miraji ni lazima mtu, kwa kuielewe
siri inayokusudiwa na herufi “B”, aihisi KWA DHATI
maana iliyokusudiwa na Bismillah!
Kwa hiyo,
hata katika swala za jamaa, haitoshi imamu kusoma
bismillah kwa niaba ya maamuma! Inabidi mtu aanze
swala kwa kuisoma mwenyewe bismillah kwa dhati na
hisia.
Yani, imamu hawezi kusema bismillah kwa niaba
ya maamuma
Ili mtu aweze kuzama ndani ya
sala inambidi achanganyike na ya Bismillah
Ni furaha iliyoje kwa mwenye kubahatika
kuchanganyika na bismillah hata mara moja kwa
siku!
Wassalaam!.
AHMED
HULUSI
10.3.2003
Raleigh - NC,
USA
|